1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUturuki

Idadi ya vifo Uturuki na Syria yapindukia watu 16,000

9 Februari 2023

Idadi hiyo inatarajiwa kuongezeka kwa kasi huku juhudi za uokoaji zikiendelea.

https://p.dw.com/p/4NH8x
Erdbeben in der Türkei und Syrien I 09.02.2023
Picha: Stoyan Nenov/REUTERS

Ikiwa yameshapita masaa 72 tangu kutokea kwa janga hilo, wataalamu wa maafa wameonesha wasiwasi wao wa kuweza kuokoa maisha zaidi.

Mamlaka zimefahamisha kuwa watu 12,873 wamekufa nchini Uturuki na takriban 3,162 katika nchi jirani ya Syria.

Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan amekiri hapo jana kuwepo mapungufu baada ya serikali yake kukosolewa kwa namna ilivyoshughulikia janga hilo.

Umoja wa Ulaya unapanga mkutano wa wafadhili mwezi Machi ili kuhamasisha misaada ya kimataifa kwa Syria na Uturuki.