1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUturuki

Erdogan akiri changamoto juhudi za uokoaji

8 Februari 2023

Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan amekiri leo kuwa kuna matatizo kuhusu namna serikali yake ilivyoanza kushughulikia tetemeko kubwa la ardhi lililotikisa kusini mwa Uturuki.

https://p.dw.com/p/4NFd6
Türkei | Präsident Recep Tayyip Erdogan in Kahramanmaras
Picha: Mustafa Kamaci /AA/picture alliance

Hayo ni wakati kukiwa na hasira kutoka kwa walioathirika na kukatishwa tamaa na kuwasili polepole kwa timu za uokozi. Erdogan ambaye atagombea katika uchaguzi wa Mei, amesema wakati alipotembelea eneo la mkasa kuwa operesheni sasa zinaendelea kama kawaida na kuahidi kuwa hakuna atakayeachwa bila makaazi. Idadi ya pamoja ya vifo nchini Uturuki na nchi jirani Syria imepanda na kupindukia watu 11,000.

Waokoaji wanaendelea kupekua vifusi vya maelfu ya majengo yaliyoporomoka kutokana na mkasa huo wa siku tatu zilizopita na kutoa miili zaidi.

Idadi ya vifo inatarajiwa kuongezeka kutoka nchi zote mbili wakati mamia ya majengo yaliyoporomoka katika miji mingi yakiwafukia watu waliokuwa wamelala majumbani mwao wakati tetemeko hilo lilipopiga saa za alfajiri.