1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ICC yamtia hatiani Ntaganda

8 Julai 2019

Mbabe wa zamani wa kivita wa Kongo, Bosco Ntaganda, amekutikana na hatia ya makosa 18 ya uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya ubinaadamu na majaji wa Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu, ICC.

https://p.dw.com/p/3LkVJ

Uhalifu huo ulitendeka wakati Ntaganda akiongoza kikosi cha waasi cha PFLC, tawi la kijeshi la chama cha UCP, kwenye jimbo la kaskazini mashariki la Ituri baina ya mwaka 2002 na 2003.