1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaHungary

Hungary yakubali kutopinga msaada wa NATO kwa Ukraine

12 Juni 2024

Serikali ya Hungary imekubali kutopinga uungaji mkono wa Jumuiya ya Kujihami ya NATO kwa Ukraine ila Waziri Mkuu Viktor Orban amesisitiza kwamba serikali yake haitatoa fedha wala wanajeshi.

https://p.dw.com/p/4gxuC
Waziri Mkuu wa Hungary Viktor Orban
Waziri Mkuu wa Hungary Viktor Orban Picha: SZILARD KOSZTICSAK/EPA

Akizungumza na waandishi wa habari, Orban amesema amemtaka Katibu Mkuu wa NATO kuweka wazi kuwa mashambulizi yoyote ya kijeshi yatakayofanywa nje ya eneo la jumuiya hiyo, yatakuwa ya hiari kulingana na sheria za NATO na tamaduni zake.

Kwa upande wake Katibu Mkuu wa jumuiya hiyo Jens Stoltenberg, amethibitisha kwamba Hungary haitoshiriki mipango ya usaidizi ya NATO kwa ajili ya Ukraine ila hakuelezea jinsi hilo litakavyofanyika.

Katika mkutano wa kilele mwezi ujao mjini Washington, Rais wa Marekani Joe Biden na wenzake wa NATO wanatarajiwa kukubaliana mfumo mpya wa kuisaidia Ukraine kwa muda mrefu kiulinzi na kulipa mafunzo jeshi lake.