1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Huenda Iraq haina silaha za kuangamiza anasema Colin Powell:

25 Januari 2004
https://p.dw.com/p/CFhK


TIFLIS: Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Colin Powell kwa mara ya mwanzo amekiri kuwa huenda Iraq haikuwa na silaha za kuangamiza kabla ya vita. Akiuzuru mji mkuu wa Georgia, Tiflis, Bwana Powell alisema hadi sasa ni hilo limebakia swali lisilojibiwa bado. Shutuma kwamba Iraq inadhibiti silaha za kuangamiza ilikuwa chanzo kikubwa kabisa katika uamuzi wa Rais George W. Bush wa Marekani wa kuipiga vita Iraq. Jumapili ya leo Waziri huyo wa Nje wa Marekani atashiriki katika sherehe ya kutawazwa madarakani Rais mpya wa Georgia Mikhail Saakashvili aliyechaguwa wiki tatu zilizopita kuwa mfuasi wa Rais aliyejiuzulu Edward Shewardnadse.