1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Hong Kong: Waandamanaji wakaidi onyo kali kutoka China

Zainab Aziz Mhariri: Jacob Safari
3 Agosti 2019

Waandamanaji wanaoipinga serikali mjini Hong Kong waliweka vizuizi katika barabara za eneo maarufu la maduka. Polisi yawataka waandamanji kuacha mara moja vitendo visivyo halali.

https://p.dw.com/p/3NHiz
Hongkong Anti-Regierungsproteste - Schild mit der Aufschrift 'Carrie Lam von der Geschichte verurteilt'
Picha: picture alliance/dpa/AP/V. Thian

Mji wa Hong Kong ambao ni wa kibiashara ulio kusini mwa China ambao umepewa mamlaka ya kujitawala kwa kiwango fulani umekabiliwa na maandamano na vurugu kwa kipindi miezi miwiili za kupinga sheria iliyopitishwa ya kuwapeleka watuhumiwa waliokamatwa Hong Kong hadi China sheria ambayo imezaa harakati pana za kutaka mageuzi ya kidemokrasia.

Waandanaji wanadai haki zaidi za kidemokrasia na uhuru wa kujitawala kwa jimbo hilo.

Mamlaka za Hong Kong na China wiki hii zilionyesha msimamo mgumu, pamoja na kukamatwa kwa waandamanaji kadhaa, huku jeshi la China likisema lipo tayari kuyamaliza machafuko hayo yasiyoweza kuvumilika iwapo litatakiwa kufanya hivyo.

Licha ya hatua hiyo ya serikali, waandamanaji hawaonyeshi ishara kwamba watalegeza kamba bali wanapanga kukusanyika kwenye maeneo mengi tofauti na kufanya mikutano wiki ijayo, hali ambayo inasababisha kuongezeka kwa mvutano huo.

Waandamanaji wanaoipinga serikali waandamana mjini Hong Kong
Waandamanaji wanaoipinga serikali waandamana mjini Hong KongPicha: Getty Images/AFP/I. Lawrence

Siku ya Jumamosi jioni, mamia ya waandamanaji waliojiziba nyuso zao waliweka vizuizi kwenye barabara za mji wa kibiashara wenye maduka mengi wa Tsim Sha Tsui, wilaya maarufu kutokana na kuwa na maduka mengi na pia kuwa ni mji wa kitalii ulio kwenye bandari. Walizuia pia mojawapo kati ya njia kuu tatu za chini kwa chini zinazoiunganisha bandari na kisiwa kikuu, na hivyo kusababisha msongamano mkubwa wa magari. Katika taarifa, polisi waliwataka raia kuepuka eneo hilo na waandamanaji nao walitakiwa waache vitendo visivyo halali.

Maandamano mawili yamepangwa kufanyika siku ya Jumapili kwenye kisiwa cha Hong Kong na katika wilaya ya Tseung Kwan O. Siku ya Jumatatu pia yamepangwa maandamano katika maeneo mengine saba. Wito wa kufanyika kwa maandamano unaonekana kuzidi kupata nguvu huku vyama vya wafanyakazi vikitangaza kujiunga na harakati hizo.

Waandamanaji wametoa wito kwa watumishi wa umma kukaa nyumbani siku ya Jumatatu kama ishara ya mshikamano na kuziunga mkono harakati za demokrasia. Walakini, wafanyakazi wa umma wanaounga mkono maandamano hayo wanajitumbukiza kwenye Vyanzo:/AFP/https://p.dw.com/p/3NHIQ