Jamii yoyote ina vielelezo vyake kama vile utamaduni na lugha. Kadri jamii inavyobadilika ndivyo vielelezo vyake vinavyobadilika. Nchini Rwanda upo wasiwasi kwamba Kinyarwanda kinaweza kubadilika mpaka kutoweka kabisa. Hiyo ndiyo mada anayoiangazia mwandishi wetu wa Kigali, Sylivanus Karemera.