1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

HELSINKI.Mchele kutoka Marekani kuchunguzwa kabla kuingizwa nchi za umoja wa ulaya

24 Oktoba 2006
https://p.dw.com/p/CCzp

Kamati ya nchi za umoja wa ulaya imesema kuwa sheria mpya itaanza hivi karibuni katika nchi hizi juu ya kufanyiwa uchunguzi mchele unaoingizwa katika nchi za umoja wa ulaya kutoka Marekani.

Nchi za umoja wa ulaya zimepitisha kwa kauli moja azimio la kufanyiwa uchunguzi mchele kutoka Marekani iwapo una viwango vinavyo kubalika kwa mujibu wa sheria za umoja huo.

Kuanzia sasa mchele kutoka Marekani utalazimika kufanyiwa uchunguzi katika maeneo yote ya viingilo kabla ya mchele huo kuingizwa katika nchi za umoja wa ulaya na hatimae kuuzwa.

Hatua hiyo imefuatia baada ya kupatikana sampuli ya mchele usiofaa katika shehena kutoka Marekani na ambao uliidhinishwa kuwa unafaa kwa matumizi ya soko la ulaya.