1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Havana. Picha mpya za Castro zatangazwa.

3 Septemba 2006
https://p.dw.com/p/CDFn

Picha mpya zimetangazwa zinazomwonyesha kiongozi wa Cuba Fidel Castro akikutana na rais wa Venezuela Hugo Chavez. Castro kwa muda alitoa madaraka kwa mdogo wake mwezi mmoja uliopita baada ya kufanyiwa upasuaji katika utumbo.

Castro amekuwa akisema mara kwa mara kuwa anamuona Chavez kuwa mrithi wa mapambano ya kimapinduzi katika eneo hilo.