1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaMarekani

Harris atoa mapendekezo ya kushusha gharama za maisha

17 Agosti 2024

Makamu wa Rais wa Marekani Kamala Harris ametangaza msururu wa mapendekezo ya kiuchumi yanayolenga kuwapunguzia Wamarekani wengi gharama za makazi, vyakula na mahitaji mengine muhimu.

https://p.dw.com/p/4jZRR
Uchaguzi nchini Marekani
Mgombea wa urais nchini Marekani Kamala Harris anataka uboresha hali ya maisha ya watu wa taifa hilo ikiwa atakuwa raisPicha: Charles Rex Arbogast/AP/dpa/picture alliance

Kwenye hotuba yake aliyoitoa kwenye jimbo la North Carolina, Harris anayegombea urais kupitia chama cha Democratic ameahidi kutilia kipaumbele kuliinua kundi la kipato cha kati katika utawala wake.

Harris, pamoja na mapendekezo yanayolenga kupunguza gharama za vyakula, amependekeza pia msaada wa kifedha kwa wanaonunua nyumba kwa mara ya kwanza na namna ya kuzisaidia familia kwa ujumla.

Mapendekezo hayo kwa kiasi kikubwa yanahitaji kuidhinishwa na bunge, hatua ambayo hata sio nyepesi katika mazingira ya sasa ya kisiasa.