1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

HAMBURG: Kansela Merkel asifu juhudi za kulinda mazingira

7 Machi 2007
https://p.dw.com/p/CCLd

Kansela wa Ujerumani Angela Merkel amesema,Umoja wa Ulaya una dhima ya kuongoza katika juhudi za kulinda mazingira duniani.Katika mahojiano yake ametoa sifa kwa nchi za Umoja wa Ulaya na halmashauri ya umoja huo,ambazo zipo tayari kuchukua hatua za kupunguza gesi ya kaboni dayoksaidi inayochafua mazingira.Siku ya Alkhamisi,suala la kuhifadhi mazingira linatazamiwa kuwa mada kuu katika mkutano wa Umoja wa Ulaya mjini Brussels.