1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Hamas: Zaidi ya wapalestina 25,000 wameuwawa Gaza

21 Januari 2024

Wizara ya afya inayoendeshwa na kundi la Hamas katika ukanda wa Gaza imesema idadi ya watu waliouwawa imefikia 25,000 wakati Israel ikiendelea na mashambulizi yake Kusini na Kaskazini mwa Gaza.

https://p.dw.com/p/4bVoT
Gaza | Mashariki ya Kati
Wizara ya afya katika Ukanda wa Gaza imesema waliouwawa huko hadi sasa wafikia 25,000Picha: DW

Israel inaendelea na mpango wake wa kulitokomeza kundi la Hamas Kusini mwa Gaza likilenga kulisambaratisha kabisa kundi hilo lililoanzisha mashambulizi yake dhidi ya Israel mnamo Oktoba 7. 

Shirika la Umoja wa Mataifa linalowashughulikia wakimbizi wa Palestina limesema watu milioni 1.7 wamepoteza makaazi yao mjini Gaza huku milioni moja wakiendelea kukusanyika katika eneo la Rafah.

Netanyahu anapinga wazo la kuipa mamlaka ya Palestina udhibiti katika ukanda wa Gaza

Mashirika ya Umoja huo yameonya kuwa kupelekwa kwa misaada katika eneo la mzozo kunahitajika haraka huku kukiwa na hatari ya watu hao kukumbwa na baa la njaa na magonjwa.