1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaMamlaka ya Palestina

Hamas iko tayari kwa mazungumzo juu ya kuachiliwa kwa mateka

24 Januari 2024

Kundi la wanamgambo la Hamas limeonyesha utayari wa kufanya mazungumzo juu ya kuachiliwa kwa baadhi ya mateka wa Israel. Hayo ni kulingana na ripoti za vyombo vya habari.

https://p.dw.com/p/4bbgt
Qatar Doha | Ismail Haniyeh
Kiongozi wa kundi la Hamas Ismail HaniyehPicha: Iranian Foreign Ministry/ZUMA Wire/IMAGO

Gazeti la The Wall Street Journal la Marekani limeripoti kuwa, Hamas imewaeleza wapatanishi kwamba wako tayari kwa mazungumzo ya kuwaachilia huru mateka wanawake na watoto kwa mabadilishano ya usitishwaji mapigano katika ukanda wa Gaza.

Wall Street Journal likinukuu maafisa wa Misri, imeendelea kueleza kuwa baadhi ya mateka wanaokusudiwa kuachiliwa huru ni pamoja na wanajeshi wanawake wa Israel.

Serikali ya Israel imeweka idadi ya mateka ambao wako hai kuwa ni takriban 105 na inaamini kwamba wengi wao wanazuiliwa katika mahandaki yanayoendeshwa na Hamas.