1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Hali nchini Kenya bado ni ya wasiwasi kufuatia maandamano

Sylvia Mwehozi
3 Julai 2024

Waandamanaji nchini Kenya, jana waliendelea na maandamano katika mji mkuu wa Nairobi na miji mingine kuhusu mswada wa fedha ambao ulikusudia kuongeza ushuru.

https://p.dw.com/p/4hnu0
Kenia | Proteste in Nairobi
Muandamanaji akishikilia bendera ya Kenya mjini NairobiPicha: Monicah Mwangi/REUTERS

Polisi waliwarushia mabomu ya kutoa machozi waandamanaji jijini Nairobi huku biashara nyingi zikiendelea kufungwa kwa hofu ya kuporwa.

Barabara kuu ya kuelekea mji wa pili kwa ukubwa nchini Kenya, Mombasa, ilifungwa huku waandamanaji wakiwasha moto. Mjini Mombasa, magari matano yalichomwa na waandamanaji nje ya hoteli ambayo mmiliki wake anadaiwa kuwafyatulia risasi waandamanaji waliokuwa wakifanya uporaji.

Soma pia: KNCHR: Watu 39 wameuawa katika maandamano ya Kenya 

Licha ya Rais William Ruto kubadili msimamo na kusema kuwa hatotia saini mswada wa fedha, baadhi ya waandamanaji sasa wanamtaka kiongozi huyo kujiuzulu na kumshutumu kwa utawala mbovu.

Lakini baadhi ya washiriki wa maandamano hayo yanayoongozwa na vijana wameelezea wasiwasi wao kwamba baadhi ya Wakenya wanatumia maandamano kufanya vurugu.