1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KNCHR: Watu 39 wameuawa katika maandamano ya Kenya

2 Julai 2024

Tume ya taifa ya haki za binadamu ya Kenya KNCHR imesema jumla ya watu 39 wameuawa katika maandamano ya kuipinga serikali nchini humo.

https://p.dw.com/p/4hl1T
Kenya-Maandamano-Nairobi
Afisa wa usalama akifyatua gesi ya kutoa machozi Picha: Brian Inganga/AP/dpa

Tume ya taifa ya haki za binadamu ya Kenya KNCHR imesema jumla ya watu 39 wameuawa katika maandamano ya kuipinga serikali nchini humo huku wanaharakati wakijiandaa kwa duru mpya ya maandamano wiki hii.

Takwimu hizo ni karibu mara mbili ya idadi iliyotangazwa awali na serikali, juu ya watu waliouawa wakati wakipinga muswada wa fedha wa 2024 ambao sasa umeondolewa.Ruto: "Sina hatia" na vifo vya waandamanaji

Tume ya haki za binadamu imesema kuna visa vya watu 32 waliopotea na waandamanaji 627 kukamatwa. Tume hiyo imelaani vurugu na matumizi ya nguvu kupita kiasi yaliyofanywa dhidi ya waandamanaji, wafanyakazi wa matibabu, wanasheria na waandishi wa habari.

Maandamano mapya yameitishwa na wanaharakati kuanzia leo Jumanne licha ya Rais William Ruto kutangaza wiki iliyopita kwamba hatatia saini kuwa sheria muswada huo ulio na nyongeza ya ushuru.