1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kitisho cha hali ya hewa kwa mechi ya Germany na Denmark

29 Juni 2024

Duru ya mtoano ya mashindano ya kandanda ya ubingwa wa Ulaya - UEFA Euro 2024 yanayofanyika hapa Ujerumani inaanza leo ambapo mechi mbili zitachezwa.

https://p.dw.com/p/4hfPh
Mchuano wa Euro 2024 mashabiki wa soka
Mashabiki wa timu ya Ujerumani wakilipokea basi la wachezaji wao walipowasili nje ya uwanja kabla ya mechi.Picha: Thilo Schmuelgen/REUTERS

Mechi kati ya wenyeji Ujerumani na Denmark mjini Dortmund inatarajiwa kufanyika kama ilivyopangwa licha ya kitisho cha kutokea dhoruba kali za radi.

Shirika la linalofuatilia mwenendo wa hali ya hewa la Ujerumani DWD limesema kuwa hali mbaya ya hewa inaweza kulikumba eneo hilo katika muda wa mwishoni mwa mchezo na kwamba kuongeza muda wa ziada si jambo linalopendekezwa kutoka kwa mtazamo wa hali ya hewa.

Mechi nyingine ya Jumamosi hii ni kati ya mabingwa wateteziItalia na Uswisi saa ambayo imepangwa kuanza wakati huu huko mjini Berlin haitaathiriwa na hali mbaya ya hewa.

Lakini katika maeneo ya washabiki na maeneo ya kutazama soka ya umma yanaweza kuwa yamefungwa kutokana na onyo la kutokea dhoruba.