SiasaMarekani
Haley aapa kutojiengua iwapo atashindwa kura za mchujo
24 Januari 2024Matangazo
Washirika wa Donald Trump wamemuwekea shinikizo balozi huyo wa zamani wa Marekani katika Umoja wa Mataifa kujiondoa kwenye kinyang'anyiro hicho iwapo atashindwa kwa kura nyingi.
Haley amewekeza raslimali nyingi katika jimbo hilo akitaraji kupata uungwaji mkono hasa miongoni mwa wanaompinga Trump na kushinda kura hizo za mchujo au angalau kupoteza kwa kura kidogo.
Kwa mujibu wa kura ya maoni iliyofanywa na shirika la habari la AP, wafuasi wengi wa Republican wana mashaka juu ya ushindi wa Trump katika jimbo la New Hampshire tofauti kabisa na Iowa, ambapo rais huyo wa zamani alipata ushindi katika kura za mchujo zilizofanyika wiki iliyopita.