1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaMarekani

Warepublican wa jimbo la Iowa, Marekani kuamua mgombea urais

16 Januari 2024

Kura ya kwanza ya mchujo ya kumtafuta mgombea wa urais wa chama Republican nchini Marekani imeanza usiku wa kuamkia leo kwenye jimbo la Iowa, huku rais wa zamani Donald Trump akipewa nafasi kubwa ya kuwa mshindi.

https://p.dw.com/p/4bHmi
Marekani | Kura ya mchujo huko Iowa | Chama cha Republican
Upigaji kura wa wanachama wa Republican katika jimbo la Iowa. Zoezi hilo ndiyo litaamua nani atakuwa mgombea urais wa chama hicho uchaguzi ujao wa mwezi Novemba, 2024.Picha: Kevin Dietsch/Getty Images

Zaidi ya vituo 1,600 vilifunguliwa majira ya saa moja usiku kwa saa za Marekani kwa wanachama wa Republican kuamua mwanasiasa atakayepeperusha bendera ya chama hicho kwenye uchaguzi wa mwezi Novemba mwaka huu.

Trump anayewania kuteuliwa kwa mara ya tatu kuwa mgombea, anachuana na balozi wa zamani wa Marekani kwenye Umoja wa Mataifa, Nikki Haley, na Gavana wa Jimbo la Florida, Ron DeSantis.

Trump anaongoza kura za maoni ya umma kwa zaidi ya asilimia 30 dhidi ya wagombea hao wawili katika jimbo la Iowa.