1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

HAKUNA SILAHA ZA MAANGAMIZI LIBYA:

23 Desemba 2003
https://p.dw.com/p/CFpx

TRIPOLI: Rais Muammar Gaddafi wa Libya amesema nchi yake haina silaha za maangamizi.Katika mahojiano maalum pamoja na steheni ya televisheni CNN kiongozi wa Libya amesema ingawa nchi yake ina miradi fulani na mashine kadha,haina cho chote cha kuficha.Mahojiano hayo yamefanywa siku tatu baada ya Libya kutangaza uamuzi wake wa kuwaruhusu wakaguzi wa kimataifa kuvitembelea vituo vyake muhimu.Ukaguzi wa vituo hivyo huenda ukaanza mapema wiki ijayo.