1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

HAKUNA SILAHA ZA HILAKI

23 Desemba 2003
https://p.dw.com/p/CFq8
TRIPOLI: Rais Muammar Gaddafi wa Libya amesema nchi yake haina silaha za maangamizi.Katika mahojiano maalum pamoja na stesheni ya televisheni-CNN kiongozi wa Libya amesema hakuna cho chote kile cha kufichwa ingawa Libya ina miradi fulani na mashine kadhaa.Mahojiano hayo yamefanywa siku tatu baada ya Libya kutangaza uamuzi wake wa kuwaruhusu wakaguzi wa kimataifa kuvitembelea vituo muhimu.Ukaguzi wa vituo hivyo huenda ukaanza mapema wiki ijayo.