1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiAfghanistan

Haki za wanawake zinavunjwa makusudi

6 Januari 2023

Mkuu wa shirika la haki za binaadamu, Volker Turk, ameshangazwa na kile alichotaja juhudi za kuratibiwa za wa kuwanyang'anya wanawake haki zao, akisema kuwa zitashindwa.

https://p.dw.com/p/4Lpcq
Flash-Galerie Stimmung in Afghanistan
Picha: AP

Katika mahojiano yake na shirika la habari la Ufaransa, AFP, Turk amesema unyanyasaji wa wanawake mitandaoni unaenea nchini Afghanistan na Iran. Amesema anataka kuizuru miji ya Kabul na Tehran kwa ajili ya kufanya mazungumzo ya moja kwa moja na maafisa.

Turk amesema hali ni mbaya zaidi Afghanistan. Amesema inatia wasiwasi kwamba takribani miaka 75 baada ya Azimio la Kimataifa la Haki za Binaadamu kupitishwa, juhudi za kuwanyima haki wanawake na wasichana zinaongezeka.