1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

HAKI ZA BINADAMU HAZIKUTIMIZWA:

11 Desemba 2003
https://p.dw.com/p/CFtC
BERLIN: Waziri wa kigeni wa Ujerumani Joschka Fischer amelalamika juu ya kushindwa kwa kutekelezwa haki za binadamu kote duniani.Akizungumza siku ya "Haki za Binadamu" Fischer amesema vita dhidi ya ugaidi si kisingizio cha kudharau haki za binadamu.Kwa upande mwingine Umoja wa Mataifa umetoa zawadi yake ya Haki za Binadamu kwa marehemu Sergio de Mello,aliekuwa mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa nchini Iraq.de Mello aliuawa Agosti mwaka huu katika shambulio lililofanywa dhidi ya makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini Baghdad.