1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaIsrael

Guterres: Raia wa Gaza wanakabiliwa na hali 'mbaya sana'

10 Oktoba 2023

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ameitaka Israel kuheshimu sheria za kimataifa, wakati ikifanya operesheni zake za kijeshi katika Ukanda wa Gaza

https://p.dw.com/p/4XKAq
Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa - Antonio Guterres akihutubia kikao cha 78 cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, Jumanne, Septemba 19, 2023 kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa
Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa - Antonio GuterresPicha: Mary Altaffer/AP/picture alliance

Guterres amesema amefadhaishwa na tangazo la Israel kuwa ingeweka mzingiro kamili dhidi ya ukanda huo, ikizuia kikamilifu kuingizwa kwa chakula, maji na nishati ya umeme.

Soma pia:Mzozo kati ya Israel na Hamas wazidi kutokota

Katibu Mkuu Guterres amesema anatambua uhalali wa wasiwasi wa Israel kuhusu usalama wake. 

Scholz asema vita baina ya Israel na Hamas havipaswi kuchochewa zaidi

Wakati huo huo Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz, amesema vita baina ya Israel na Hamas havipaswi kuchochea zaidi moto wa uhasama, na kuongeza kuwa ugaidi hautashinda.

Kansela wa Ujerumani - Olaf Scholz akitoa taarifa kuhusu Israel mnamo Oktoba 8, 2023
Kansela wa Ujerumani - Olaf ScholzPicha: Fabian Sommer/dpa/picture alliance

Soma pia:Mataifa mengi zaidi yanazidi kusitisha na kupitia upya misaada ya kifedha katika maeneo ya Palestina kufuatia uvamizi wake nchini Israel

Akiwa pamoja na rais wa Ufaransa Emmanuel Macron mjini Hamburg, viongozi hao wawili wamesema wanasimama pamoja na Israel.

Umoja wa Mataifa wafuta kauli ya msaada wa Wapalestina

Hayo yakiarifiwa, Umoja wa Ulaya umefuta kauli yake ya awali kuwa unasitisha msaada wa kibinadamu kwa Wapalestina. Aidha, Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu ameutaka upinzani nchini mwake kuridhia kuundwa kwa serikali ya umoja wa kitaifa bila masharti yoyote, wakati nchi hiyo ikiendelea na operesheni za kulipa kisasi dhidi ya Hamas.

Soma pia:Serikali ya Israel yawaamuru wanajeshi wake kulizingira eneo la Ukanda wa Gaza

Zaidi ya siku mbili baada ya Hamas kuanzisha mashambulizi ya kushtukiza kutokea Ukanda wa Gaza, jeshi la Israel limesema kwa kiasi kikubwa limerudisha udhibiti katika miji ya kusini ambako limekuwa likipambana na wapiganaji wa Hamas.