1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Migogoro

Ghala la mafuta la Urusi lashambuliwa na droni za Ukraine

28 Agosti 2024

Gavana wa jimbo la Rostov la kusini magharibi mwa Urusi amesema ghala la mafuta liliwaka moto baada ya kushambuliwa na ndege za droni za Ukraine.

https://p.dw.com/p/4k05K
Ghala la mafuta limeshambuliwa na Ukraine
Mkoa wa Urusi wa Rostov ambako ghala la mafuta limeshambuliwa na UkrainePicha: REUTERS

Gavana wa jimbo la Rostov la kusini magharibi mwa Urusi amesema ghala la mafuta liliwaka moto baada ya kushambuliwa na ndege za droni za Ukraine. Gavana huyo Vasily Golubev amesema wazima moto bado wanapambana na moto, lakini ameeleza kuwa hakuna nyumba zilizomo hatarini.Urusi yapambana kuuzima moto unaowaka kwa siku ya tatu kwenye ghala ya mafuta

Tangu kuanza kwa vita mnamo mwaka 2022 Ukraine imekuwa inazilenga sehemu za Urusi za kuhifadhia mafuta na gesi katika kile inachoita visasi halali katika kulipiza mashambulio yanayofanywa na Urusi kwenye miundombinu ya nishati ya Ukraine. Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky, ameyasifu majeshi yake kwa kuzishambulia sehemu za nishati za Urusi na ameeleza kuwa mashambulio hayo yatasaidia juhudi za kuvimaliza vita kwa njia ya haki.