1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroUrusi

Urusi yapambana kuuzima moto kwenye ghala ya mafuta

20 Agosti 2024

Mamia ya wazaima moto wanapambana na moto mkubwa kwenye jimbo la Rostov kaskazini mwa Urusi.

https://p.dw.com/p/4jfYf
Urusi l Moto wawaka kwenye ghala ya mafuta
wazima moto wakiwa katika harakati za kuudhibiti moto uliowaka kwenye ghala ya mafuta Picha: Russia Emergency Ministry/dpa/picture alliance

Moto huo umesababishwa na shambulio lililofanywa na ndege za droni za Uraine kwenye bohari ya mafuta katika mji wa Proletarsk.

Urusi imesema wazima moto kadhaa wamejeruhiwa. Wazima moto wapatao 520  wanapambana na moto huo ambao umezagaa kwenye eneo la kilometa za mraba 10,000.

Gavana wa Rostov Vasily Golubev amesema wazima moto 41 wanapata matibabu, huku wengine kadhaa wakiwa na majeraha ya moto.

Hakuna raia aliyeripotiwa kujeruhiwa.