1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ghala la jeshi la Chad laripuka

19 Juni 2024

Moto mkubwa umezuka katika ghala kubwa la kijeshi katika mji mkuu wa Chad, N'Djamena, na kusababisha miripuko mikubwa iliyoyatikisa majengo yaliyokuwa umbali wa hadi kilomita saba kutoka eneo hilo.

https://p.dw.com/p/4hF7J
Mahamat Idriss Deby
Rais Mahamat Idriss Deby wa Chad.Picha: Israel Matene/REUTERS

Bila kutoa idadi kamili, Rais Mahamat Idriss Deby Itno katika ujumbe aliouandika kwenye mtandao wa kijamii wa Facebook, amesema watu kadhaa wamepoteza maisha na kujeruhiwa kutokana na mripuko huo.

Moto huo unadaiwa kuzimwa baada ya saa sita usiku.

Soma zaidi: Moto wateketeza hifadhi kubwa ya silaha za jeshi mji mkuu wa N'Djamena

Waziri wa Mambo ya Nje, Abderaman Koulamallah, pia amesema kwamba kulikuwa na miripuko kadhaa na akawataka raia wawe watulivu.

Kulingana na shahidi mmoja aliyezungumza na shirika la habari la AFP, miripuko hiyo ililiharibu paa la nyumba yake na yeye na watoto wake wakalazimika kutafuta hifadhi maeneo mengine kwa hofu kwamba nyumba zao zingeporomoka.