1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiChad

Moto wateketeza hifadhi kubwa ya silaha ya jeshi Chad

19 Juni 2024

Moto mkubwa umezuka jana jioni kwenye ghala la kuhifadhi silaha za jeshi katika mji mkuu wa Chad, N'Djamena.

https://p.dw.com/p/4hDxN
Israel, Safad | Feuer nach Rakatenbeschuss aus dem Libanon
Picha: Atef Safadi/EPA

Waziri wa mambo ya nje ambaye pia ni msemaji wa serikali Abderaman Koulamallah ameandika kwenye mtandao wake wa kijamii wa Facebook kuwa, kumetokea mlipuko mkubwa kwenye ghala la silaha za jeshi na amewahimiza watu kuwa watulivu.

Koulamallah hata hivyo hakueleza chanzo cha moto huo au idadi ya majeruhi.

Mkasa huo wa moto pia umethibitishwa na afisa mwandamizi wa jeshi aliyeliambia shirika la habari la AFP kuwa, ghala kubwa zaidi la kuhifadhi silaha liliko mjini N'Djamena limeteketea kwa moto.

Soma pia: Chad yatangaza serikali mpya baada ya utawala wa kijeshi 

Hifadhi hiyo ya silaha iko upande wa kaskazini mwa mji mkuu N'Djamena karibu na uwanja wa ndege wa kimataifa. N'Djamena ni nyumbani kwa takriban watu milioni 1.6 ambao ni karibu asilimia 10 ya idadi jumla ya watu nchini Chad.

Waandishi wa shirika la habari la AFP wamesema milipuko ilisikika kutoka hifadhi hiyo ya silaha ilioko karibu na uwanja wa ndege na kwamba silaha zimeteketea.