1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Georgia kufanya kura ya maoni kuhusu kujiunga na NATO

27 Novemba 2007
https://p.dw.com/p/CTXc

Georgia imetangaza itafanya kura ya maoni mwezi Januari mwakani kuhusu kutaka kujiunga na jumuiya ya kujihami ya kambi ya magharibi, NATO.

Jamhuri hiyo ya muungano wa zamani wa Sovieti, ni mwanachama wa mpango wa ushirikiano kwa amani wa jumuiya ya NATO, na imelifanyia marekebisho jeshi lake kupitia msaada wa Marekani.

Urusi inapinga vikali kupanuliwa kwa jumuiya ya NATO katika muungano wa zamani wa Sovieti.

Kura ya maoni itakayofanyika terehe 5 Januari mwaka ujao, itafanyika sambamba na uchaguzi wa bunge nchini Georgia, baada ya rais Mikhail Saakashvili, anayependelea ushirikiano wa karibu na Marekani, kuitisha uchaguzi wa mapema na kujiuzulu wiki iliyopita.