1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaMexico

Genge la madawa ya kulevya lauwa 6, lajeruhi 12 Mexico

13 Julai 2023

Watu sita wameuawa na wengine 12 wamejeruhiwa katika mashambulizi ya magenge ya madawa ya kulevya yaliyowalenga maafisa wa usalama magharibi mwa Mexico katika mji wa Guadalajara jimbo la Jalisco.

https://p.dw.com/p/4ToVU
Mexiko | Polizeieinsatz
Picha: Bernandino Hernandez/AP/picture alliance

Gavana wa jimbo hilo, Enrique Alfaro, amesema ni kitendo cha kikatili na kigaidi ambacho hakijawahi kushuhudiwa licha ya kuwa anaongoza moja ya majimbo yenye vurugu sana nchini Mexico. 

Soma zaidi: Raia wawili wa Marekani wauwa Mexico

Gavana huyo amelaani kitendo hicho lakini akashindwa kulitaja moja kwa moja genge la walanguzi wa dawa za kulevya linaloogopwa mno nchini Mexico la Jalisco New Generation.

Soma zaidi: 2020: Ongezeko la mauaji yanayolenga waandishi habari

Mashambulizi hayo ya mabomu yanahusishwa na biashara haramu ya dawa za kulevya, jambo ambalo kwa miongo kadhaa limekuwa tatizo kubwa nchini Mexico.

Soma zaidi: El-Chapo afungwa maisha

Tangu kuanza kwa mwaka huu, watu 1,095 wameuawa na wengine 750 wamepotea katika mazingira ya kutatanisha.