1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

GENEVA Raia wa Uswisi waunga mkono marufuku ya sheria za mipaka

6 Juni 2005
https://p.dw.com/p/CF6e

Wapigaji kura nchini Uswissi wameunga mkono kupigwa marufuku kwa sheria za mipakani kufikia mwaka 2007 kupitia kura ya maoni. Asilimia 55 ya wapigaji kura wameiunga mkono serikali katika mpango wake wa kujiunga na eneo la Schengen, ambalo linayajumulisha mataifa 13 wanachama wa umoja wa Ulaya, yakiwemo Iceland na Norway.

Raia wa mataifa haya wana uhuru wa kuvuka mipaka ya mataifa hayo pasipo kuwa na viza za kusafiria kutoka kwa ofisi za ubalozi. Uswissi imekataa kujiunga na jumuiya ya Ulaya licha ya kuzungukwa na mataifa ya jumuiya hiyo.

Katika kura tofauti ya maoni, wapigaji kura pia wameziidhinisha sheria mpya zinazowaruhusu wanaume waliooana kuwa na haki zaidi katika jamii na kulipa kodi sawa na wanaume na wanawake wanaoishi katika ndoa.