1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

GENEVA: Matatizo ya ujauzito na uzazi yauwa wanawake

8 Aprili 2005
https://p.dw.com/p/CFPV

Kila mwaka kiasi ya wanawake nusu milioni hufariki sehemu mbali mbali za dunia kwa sababu ya matatizo yanayotokea wakati wa ujauzito na uzazi,na hali maisha hayo yangeweza kuokoleka.Hiyo ni kwa mujibu wa ripoti ya Shirika la Afya Duniani la Umoja wa Mataifa-WHO iliyotolewa kuadhimisha siku ya Afya Duniani.Ripoti hiyo inasema watoto wachanga pia wapatao milioni 4 hufariki katika wiki ya mwanzo ya kuzaliwa kwao.Wengi wangéweza kunusurika kwa misaada midogo kama ya kupatiwa maji,kupewa maziwa ya mama pamoja na dawa za kimsingi.Kwa upande mwingine Msumbiji imesema mwaka huu inatazamia kutoa chanjo dhidi ya polio na surua kwa watoto milioni 9.