1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiGambia

Gambia yashikilia uamuzi wa kupiga marufuku ukeketaji

16 Julai 2024

Shirika la afya duniani WHO na lile la kuwahudumia watoto UNICEF wametoa taarifa ya pamoja wakiipongeza Gambia kwa hatua ya kuzuia muswada uliolenga kuondoa marufuku ya wanawake kukeketwa.

https://p.dw.com/p/4iM8L
Ukeketaji wa wanawake Gambia
Bunge la Gambia limetupilia mbali mswada uliolenga kuondoa marufuku ya ukeketaji wa wanawakePicha: Malick Njie/REUTERS

Shirika la afya duniani WHO na lile la kuwahudumia watoto UNICEF wametoa taarifa ya pamoja Jumatatu jioni wakiipongeza Gambia kwa hatua ya kuzuia muswada uliolenga kuondoa marufuku ya wanawake kukeketwa.

Mashirika hayo ya kimataifa yamesema hatua hiyo inathibitisha kwa mara nyingine ahadi za Gambia katika masuala ya haki za binadamu, usawa wa kijinsia, na kulinda afya na ustawi wa wasichana na wanawake.

Wabunge nchini Gambia walipiga kura ya kutupilia mbali muswada huo. Mwaka 2015, kiongozi wa zamani wa Gambia Yahya Jammeh alipiga marufuku vitendo vya ukeketaji, lakini wanaharakati wanasema utekelezaji wa sheria hiyo umekuwa dhaifu na wanawake wanaendelea kufanyiwa vitendo hivyo.