1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Frankfurt: Lufthansa kununua kampuni ya ndege ya SWISS

6 Julai 2005
https://p.dw.com/p/CEwx

Kampuni ya ndege ya Ujerumani, Lufthansa, itainunua kampuni ya ndege ya Uswissi, SWISS. Tume ya Ulaya imelikubali jambo hilo baada ya idara ya Marekani inayosimamia biashara kuukubali ununuzi huo. Makampuni hayo mawili yalitakiwa yaachane na haki yao ya kuruka na kutuwa katika viwanja vya ndege vinane, pindi mashirika yanayoshindana nayo yakitaka. Pia Lufthansa imekubali kuachana na mipango yake ya kuzidisha idadi ya safari zake katika baadhi ya njia.