1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Felix Tshisekedi aongoza kwenye matokeo ya awali Kongo

26 Desemba 2023

Zoezi la kuhesabu kura linaendelea nchini Jamhuri ya Kidemokraisa ya Kongo siku sita baada ya uchaguzi mkuu uliogubikwa na kashfa za wizi wa kura na kucheleweshwa kusambazwa vifaa vya uchaguzi.

https://p.dw.com/p/4aa8h
Uchazuzi DRC
Denis Kadima, Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (CENI),(Aliyevalia shati Jeupe na kofia).Picha: JUSTIN MAKANGARA/REUTERS

Mwenye kiti wa Tume ya uchaguzi CENI, Denis Kadima amesema tume hiyo haitosita kufuta baadhi ya matokeo ya uchaguzi iwapo udanganyifu utathibitishwa. Kadima amesema vurugu zilizotokea siku ya uchaguzi hazikupangwa na CENI na amewatupia lawama baadhi ya wanasiasa ambao walijaribu kuiba kura kwa kushirikana na baadhi ya mawakala wa tume ya uchaguzi.

Soma pia: Upinzani Kongo wapanga kufanya maandamano kulalamikia kasoro za uchaguzi

Hadi jana Jumatatu baadhi ya maeneo yaliendelea kupiga kura, ikiwa ni siku tano baada ya uchaguzi kufanyika. Tume ya uchaguzi imeelezea hatua hiyo inalenga kuwapa fursa wapiga kura wote ambao vifaa vya uchaguzi vilichelewa kufikishwa kwenye maeneo yao tarehe 20 Desemba.

Soma pia: Kwa nini uchaguzi ni muhimu DR Kongo?

Tume ya Uchaguzi kufikia sasa imetangaza matokeo ya kura milioni 1.9, kati ya jumla ya wapiga kura milioni 44 waliojiandikisha. Na rais Felix Tshisekedi anayewania muhula wa pili anaongoza kwenye matokeo hayo ya awali.