1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Nahodha wa Real Madrid Nacho atangazwa kuondoka klabuni humo

25 Juni 2024

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 34, kwa sasa yuko Ujerumani na kikosi cha Uhispania kushiriki kombe la Euro 2024, ameshinda mataji mengi makubwa akiwa na Madrid kuliko mchezaji mwingine yeyote

https://p.dw.com/p/4hVAM
Real Madrid
Nahodha wa Real Madrid anaondoka klabuni humo katika mjira haya ya joto.Picha: Carl Recine/REUTERS

Mabingwa wa Ulaya, Real Madrid wamemtangaza nahodha Nacho kuondoka kwenye klabu hiyo kwenye majira haya ya joto.

Beki huyo ataondoka Santiago Bernabeu huku kukiwa na uvumi kuwa yuko tayari kujiunga na klabu ya Saudi Pro League Al Qadsiah mkataba wake utakapoisha.

Soma zaidi. EURO 2024: Italia wailazimisha Croatia sare 1-1 huku Albania ikifungwa na Uhispania

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 34, kwa sasa yuko Ujerumani na kikosi cha Uhispania Euro 2024, ameshinda mataji mengi makubwa akiwa na Madrid kuliko mchezaji mwingine yeyote.

 Borussia Dortmund - Real Madrid -
Nahodha wa Real Madrid Nacho akishangilia goli katika mchezo wa fainali ya ligi ya mabingwa uliochzewa Wembley na mwenzake Dani CarvajalPicha: Sarah Meyssonnier/REUTERS

Taarifa ya klabu ilisema: "Real Madrid CF inatangaza kuwa nahodha wetu Nacho ameamua kumalizia soka lake kama mchezaji wa Real Madrid. "Real Madrid ingependa kutoa shukrani na upendo kwa Nacho, mmoja wa magwiji wa klabu yetu."

Soma zaidi. Ufaransa yalazimishwa sare ya 0-0 na Uholanzi, bila Mbappe

Nacho alijiunga na akademi ya Madrid mwenye umri wa miaka 10 na alicheza kwa mara ya kwanza katika kikosi cha kwanza mwaka 2012. Kwa muda wote huu amecheza michezo 364 na kushinda mataji 26. Makombe Sita ya ligi ya mabingwa Ulaya, Matano pia ya Klabu Bingwa vya Dunia, Vikombe vinne vya Uropa, Vikombe vinne vya ligi, mawili ya kombe la Copa del Rey na matano ya kombe la Spanish Super Cup.