1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

EURO 2024: Maandalizi yaendelea kushika kasi

3 Juni 2024

Timu ya taifa ya kandanda ya Ujerumani ina matumaini ya kuandikisha matokeo mazuri katika ardhi ya nyumbani ili kuwavutia mashabiki zaidi wa nyumbani na kurudisha hadhi yao kimataifa.

https://p.dw.com/p/4gavk
Kocha wa Ujerumani Nagelsmann
Picha ya kubuni inayomuonyesha kocha wa timu ya taifa ya Ujerumani Julian Nagelsmann mbele ya kombe la EURO 2024.Picha: Thomas Boecker/DFB/Sven Simon/IMAGO

Mabingwa hao mara tatu wa Ulaya kukamilisha muongo mmoja bila ya taji lolote kuu.

Baada ya kuondolewa katika fainali mbili za Kombe la Dunia la 2018 na 2022 katika awamu ya makundi, ikiwa rekodi mbaya zaidi ndani ya miaka 80, pamoja na kuondolewa kwenye michuano ya Euro hatua ya 16 bora miaka mitatu iliyopita. Wakati huu kocha Julian Nagelsmann anatarajia kubadilisha mkondo na kurudisha heshima ya Ujerumani kuanzia mechi ya ufunguzi dhidi ya Scortland Juni 14.

Soma pia: EURO 2024: Kikosi cha Uholanzi

Hii leo Ujerumani inashuka dimbani kuchuana na Ukraine katika mechi ya kirafiki, huku kocha Nagelsmann akithibitisha kuwa mlinda lango Manuel Neur atarejea kikosi baada ya kuwa nje kwa muda kutokana na matatizo ya tumbo.

"Bila shaka, matatizo hayo ya tumbo yanachosha. Ndio maana alipewa siku mbili za kutibu ugonjwa wake. Amecheza michezo mingi na yuko katika hali mzuri, na pia ameonyesha umakini   mazoezini."

"Jambo zuri ni kwamba huna haja ya kumueleza chochote kuhusu mechi. Tayari anaelewa kila kitu. Kimwili, yuko katika hali nzuri, amefanya mazoezi vizuri na hakika atacheza mchezo mzuri ."

Soma pia: Toni Kroos kutundika daluga baada ya EURO 2024

Haya yajiri huku Nagelsmann akikosoa uchunguzi wenye utata uliofanywa kabla ya mashindano ya Euro, ambao umedai kuwa mmoja kati ya Wajerumani watano wangependelea kuona wachezaji wazungu wakiiwakilisha timu ya taifa ya Ujerumani.

Kikosi rasmi cha wachezaji 27 cha Ujerumani kinajumuisha idadi ya wachezaji walio na usuli wa uhamaji.

Uhispania kuzima kelele za RFEF

Luis de la Fuente | Kocha wa timu ya taifa ya Uhispania
Uhispania yapania kuzima kelele na migogoro ya shirikisho la soka RFEF.Picha: Flaviu Buboi/NurPhoto/IMAGO

Timu ya taifa ya Uhispania itawasili Ujerumani wakitaka kujiimarisha tena kama washindani wakuu wa taji huku wakitumai kuzima kelele baada ya miezi kadhaa ya mabishano yanayohusu shirikisho la soka la nchi hiyo (RFEF).

Kocha Luis de la Fuente na wachezaji wake wamelazimika kukabiliana na migogoro  inayoizunguka RFEF, lakini anasema kikosi chake kipo imara kwa kuwajumuisha wachezaji Lamine Yamal, Pau Cubarsi, kiungo wa Manchester City Rodri, Dani Carvajal wa Real Madrid na Alvaro Morata wa Atletico Madrid.

England ipo tayari

EURO 2020 | Harry Maguire| Luke Shaw
Wachezaji wa England Harry Maguire na Luke Shaw watakua imara kushiriki Euro 2024.Picha: Alberto Lingria/REUTERS

Kikosi cha England, Kocha Gareth Southgate ametiwa moyo na maendeleo ya Harry Maguire na Luke Shaw mabeki waliojeruhiwa wanaoendelea kupata nafuu na amethibitisha kuwa wako katika hali njema kushiriki kwa Euro 2024.

Maguire, kiungo mkabaji muhimu kwa England kutokana na kutokuwa na chaguo katika nafasi hiyo, amekuwa nje kwa mwezi mmoja, huku beki wa kushoto Shaw akiwa  nje kwa miezi mitatu.

Sikiliza pia:

Uhispania yapania kuzima kelele za RFEF

Kombe la EURO 2024 Ujerumani