1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MichezoUholanzi

EURO 2024: Kikosi cha Uholanzi

30 Mei 2024

Kocha wa timu ya taifa ya kandanda ya Uholanzi Ronald Koeman ataja kikosi kitakachowakilisha Uholanzi kwenye mashindano ya EURO 2024 nchini Ujerumani.

https://p.dw.com/p/4gSyW
Kandanda I EURO 2024
Kocha wa timu ya taifa ya kandanda ya Uholanzi Ronald Koeman.Picha: Armando Franca/AP/picture alliance

Kocha Ronald Koeman amemjumuisha kiungo wa kati wa Barcelona Frenkie de Jong katika kikosi chake cha mwisho cha wachezaji 26 kwa ajili ya mashindano ya Euro 2024 licha ya kwamba bado anauguza jeraha la kifundo cha mguu.

Koeman hata hivyo amemuacha nje beki wa kushoto Ian Maatsen, ambaye amekuwa na mchango mkubwa katika maendeleo ya Borussia Dortmund hadi fainali ya Ligi ya Mabingwa dhidi ya Real Madrid Jumamosi (01.06.2024) lakini hajawahi kujumuishwa kwenye timu ya wachezaji wakubwa ya nchi yake.

Soma pia:Ujerumani inaweza kufanya vyema EURO 2024

Kocha huyo ameweka imani yake kwa beki wa kushoto kati ya wachezaji wawili, Nathan Ake, ambaye alishinda taji la Ligi Kuu akiwa na Manchester City, na mkongwe Daley Blind.

De Jong alipata jeraha katika kipigo cha 3-2 cha Barcelona kutoka kwa Real Madrid kwenye Clasico mnamo Aprili 21 mara ya tatu msimu huu kuugua kifundo cha mguu lakini anatarajiwa kurejea mazoezini Jumamosi, chini ya wiki mbili kabla ya mechi za kombe la Euro kuanza.

Kuna wasiwasi pia kuhusu kiwango cha mshambuliaji wa Athletico Madrid Memphis Depay.

Uholanzi, ambao wamewahi kutwaa taji la Ulaya mara moja mwaka 1988, wako Kundi D pamoja na Ufaransa, Austria na Poland. Lakini kwanza wanajiandaa kucheza na Canada Juni 6 na Iceland kunoa makali yao.

Kikosi:

Kandanda Kombe la Dunia 2022 Qatar | Kikosi cha Uholanzi
Kikosi cha timu ya taifa ya kandanda ya Uholanzi, wakipiga picha wakati wa mashindano ya Kombe la Dunia 2022 katika uwanja wa Lusail Qatar.Picha: Ariel Schalit/AP Photo/picture alliance

Walinda lango: Justin Bijlow (Feyenoord), Mark Flekken (Brentford), Bart Verbruggen (Brighton).

Mabeki: Nathan Ake (Manchester City), Daley Blind (Girona), Stefan de Vrij (Inter Milan), Lutsharel Geertruida (Feyenoord), Denzel Dumfries (Inter Milan), Matthijs de Ligt (Bayern Munich), Jeremie Frimpong (Bayer Leverkusen), Micky van de Ven (Tottenham Hotspur), Virgil van Dijk (Liverpool).

Viungo: Frenkie de Jong (Barcelona), Ryan Gravenberch (Liverpool), Teun Koopmeiners (Atalanta), Tijjani Reijnders (AC Milan), Jerdy Schouten (PSV Eindhoven), Xavi Simons (RB Leipzig ), Joey Veerman (PSV Eindhoven), Georginio Wijnaldum (Al Ettifaq).

Washambuliaji: Steven Bergwijn (Ajax), Brian Brobbey (Ajax), Memphis Depay (Atletico Madrid), Cody Gakpo (Liverpool), Donyell Malen (Borussia Dortmund), Wout Weghorst (Hoffenheim)

     

Kombe la EURO 2024 Ujerumani