1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

EU yasema itaweka ulinzi dhidi ya ukiukaji wa Urusi katika

2 Aprili 2023

Mkuu wa sera za Kigeni wa Umoja wa Ulaya Josep Borrell amesema umoja huo utaweka ulinzi dhidi ya ukiukaji wowote wakati wa muhula wa urais wa Urusi wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa katika mwezi wa Aprili.

https://p.dw.com/p/4PbW6
USA New York | UN-Sicherheitsrat
Picha: Ed Jones/AFP/Getty Images

Urusi, moja ya wanachama watano wa kudumu wa Baraza la Usalama, jana imechukua urais wake kama sehemu ya mapokezano ya kila mwezi kati ya wanachama wake 15.

Borrell amesema licha ya kuwa mwanachama wa kudumu wa Baraza la Usalama, Urusi imeendelea kukiuka kiini chenyewe cha mfumo wa kisheria wa Umoja wa Mataifa.

Ukraine ilisema urais wa Urusi katika Baraza la Usalama ni kama tusi. Moscow ilikuwa mwenyekiti wa baraza hilo Februari 2022, mwezi ambao iliivamia Ukraine, na kuifanya Kyiv kutoa wito wa kuondolewa Urusi kwenye baraza hilo.