1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

EU, Ujerumani zataka Poland kujieleza kuhusu rushwa ya visa

20 Septemba 2023

Umoja wa Ulaya na Ujerumani zimeiongezea shinikizo serikali ya Poland kutoa ufafanuzi juu ya kashfa kubwa ya utoaji viza inayoweza kuwa na athari mbaya kwa majirani zake katika Umoja wa Ulaya.

https://p.dw.com/p/4WblY
Vyombo vya habari vya Poland, vimeripoti kwamba mfumo unaowalazimimisha raia kutoka Mashariki ya Kati na Afrika kutoa rushwa ili kupewa visa za Umoja huo.
Vyombo vya habari vya Poland, vimeripoti kwamba mfumo unaowalazimimisha raia kutoka Mashariki ya Kati na Afrika kutoa rushwa ili kupewa visa za Umoja huo.Picha: Nikolai Sorokin/Zoonar/picture alliance

Wakati hali ya mvutano ikiongezeka ndani ya Umoja huo kuhusiana na mzozo wa uhamiaji, waziri wa mambo ya ndani wa Ujerumani Nancy Faeser jana Jumanne alimpigia simu mwenzake wa Poland Mariusz Kaminski, na wizara yake ikimtaka balozi wa Warsaw mjini Berlin kuzungumzia sakata hilo.

Vyombo vya habari vya Poland, vimeripoti kwamba mfumo unaowalazimimisha raia kutoka Mashariki ya Kati na Afrika kutoa rushwa ili kupewa visa za Umoja huo, maarufu Schengen umewekwa kwenye balozi ndogo za Poland pamoja na makampuni ya nje yaliyoko kwenye mataifa husika.

Kwenye mazungumzo, Berlin imeitaka Warsaw kutoa ufafanuzi wa haraka, uliokamilika na wa kina juu ya madai hayo, huku Umoja wa Ulaya ukiipatia wiki mbili za kujieleza na kuziita ripoti hizo kuwa ni za kutia wasiwasi mkubwa.