1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ethiopia yafuta mashitaka dhidi ya viongozi wa waasi wa TPLF

31 Machi 2023

Serikali ya Ethiopia hapo jana imetangaza kuwaondolea mashtaka ya uhalifu viongozi wa Chama cha Ukombozi wa Watu wa Tigray TPLF, kama ilivyoainishwa katika mpango wa amani kaskazini mwa nchi hiyo

https://p.dw.com/p/4PYAL
Äthiopien Friedensabkommen Tigray
Picha: PHILL MAGAKOE/AFP/Getty Images

Serikali ya Ethiopia hapo jana imetangaza kuwaondolea mashtaka ya uhalifu viongozi wa Chama cha Ukombozi wa Watu wa Tigray TPLF, kama ilivyoainishwa katika mpango wa amani kaskazini mwa nchi hiyo.

Tangazo hilo lililotolewa na wizara ya sheria ya Ethiopia ni hatua ya hivi karibuni inayoonesha imani iliyoko katika mkataba huo wa amani.

Wiki iliyopita, serikali ya Ethiopia ilisema imemteua afisa mmoja mwandamizi wa TPLF kuwa mkuu wa utawala wa mpito wa Tigray. Uteuzi huo ulifanyika siku moja tu baada ya bunge la nchi hiyo kuliondoa kundi la TPLF katika orodha rasmi ya makundi ya kigaidi.

Mgogoro wa Tigray ulianza Novemba 2020 pale Waziri Mkuu Abiy Ahmed alipoyatuma majeshi Tigray kuuangusha uongozi wa TPLF akiwashutumu wapiganaji wake kwa kushambulia kambi za kijeshi za shirikisho.