1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ethiopia na Eritrea zatia saini mkataba wa urafiki

17 Septemba 2018

Ethiopia na Eritrea zaimarisha makubaliano yao ya amani kwa kutia saini mkataba wa urafiki nchini Saudi Arabia

https://p.dw.com/p/34z8f
Saudi Arabien Äthiopien und Eritrea schließen Freundschaftsvertrag
Picha: picture-alliance/AP Photo/SPA

Miezi miwili baada ya kutiliana saini makubaliano ya kihistoria ya kurejesha amani kati yao,  Ethiopia na Eritrea zimetiliana saini mkataba wa urafiki.

Rais Isaias Afwerk wa Eritrea na Waziri Mkuu wa Ethiopia, Abiy Ahmed, walitia saini mkataba huo mjini Jeddah mbele ya mfalme wa Saudi Arabia, Salman bin Abdulaziz Al Saud.

Hata hivyo, hakuna maelezo ya undani juu ya mkataba huo yaliyotolewa. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres pia alihudhuria sherehe hiyo ya kutia saini.