1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
UchumiEthiopia

Ethiopia kuruhusu wageni kumiliki mali zisizohamishika

24 Machi 2024

Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed amesema taifa hilo linanuia kupitisha sheria itakayowaruhusu wageni kumiliki mali zisizohamishika.

https://p.dw.com/p/4e4WW
Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahimed
Abiy Ahmed akiwa kwenye mjadala wa wazi na wawakilishi kadhaa wa jumuiya mbalimbali. Picha hii ni kwa hisani ya Ofisi ya Waziri Mkuu wa Ethiopia - Addis Ababa-22.03.2024Picha: Office of Prime minister of Ethiopia

Kituo cha televisheni ya taifa kimeripoti jana Jumamosi kwamba Abiy ameuambia mkutano wa walipa kodi wakubwa katika mji mkuu Addis Ababa kwamba serikali yake iko mbioni kuhitimisha sheria mpya itakayoruhusu wageni kumiliki mali hiyo ingawa hakusema ni lini itapelekwa bungeni.

Hivi sasa wageni hawaruhusiwi kumiliki nyumba nchini Ethiopia, iwe ni jengo la makazi au biashara, jambo linaloonekana kuwa kizuizi katika juhudi zinazoendelea za kuwavutia wawekezaji wa kigeni kwenye taifa hilo la Pembe ya Afrika.