1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ETA yasitisha matumizi ya silaha

Maja Dreyer23 Machi 2006

Chama cha waasi ETA katika jimbo la Basque, Kaskazini mwa Uhispania, jana usiku kiliarifu kuwa kitakubali kusitisha mapigano ya silaha kuanzia Ijumaa hii. Bado lakini wahariri wa magazeti ya Ujerumani wanaona kuna wasi wasi juu ya malengo ya waasi hawa.

https://p.dw.com/p/CHWZ

Pamoja na hayo, magazeti oia yanaiangalia Afghanistan ambako mtu mmoja aliyeingia Ukristo alifikishwa mahakamani baada ya kutanasari kutoka dini ya Kiislamu. Gazeti la “Nürnberger Zeitung” linazionya nchi za Magharibi kutoonyesha hisia kali mno.

Limeandika: “Bila shaka haiwezekani kwamba katika nchi yoyote inayolinda haki za watu walio wachache ,Mkristo anauawa kwa sababu ya dini yake. Lakini katiba ya Afghanistan iliyosifiwa na jumuiya ya kimataifa, pia inasema kuwa Muislamu haruhusiwi kuingia katika dini nyingine. Ikiwa sheria hiyo hata hivyo itaruhusu hukumu hafifu inategemea diplomasia ya taratibu badala ya kelele zinazosikika hivi sasa.”

Na mhariri wa gazeti la “Handelsblatt” la mjini Düsseldorf ameandika:
“Kesi hii inaonyesha kazi ngumu na ndefu ya kuiimarisha demokrasia katika nchi husika. Faida za demokrasia na kutekeleza haki za binadamu si mambo yanayoweza kushinikizwa kutoka juu. Inabidi jamii ya Afghanistan ifahamu na iunge mkono haki hizi ili upinzani dhidi ya kesi ya Mkristo huyu usisikike sio tu mjini London au Berlin lakini pia kwenye mabarabara za Kabul!”

Katika gazeti la “Berliner Zeitung” tunasoma maoni yafuatayo:
“Yule ambaye anaonyesha wasi wasi juu ya jeshi la Ujerumani kukaa nchini Afhanistan baada ya kesi hii dhidi ya Mkristo Abdul Rahman, anazungumzia bila kufikiri. Jeshi liko Afghanistan kwa muda ili kuhakikisha maendeleo ya demokrasia nchini humo. Huwezi kuyaelemisha makabila ya Afghanistan yahemishu dini nyingine katika siku moja tu. Na pia, Hamid Karsai anaongoza nchi ya Afghanistan ya Waafghanistan wenyewe na siyo Ujerumani inayojaa marafiki wa haki za binadamu.”

Na mada nyingine inayohusika na taarifa ya kundi la waasi wa jimbo la Basque nchini Uhispania, ETA, kusitisha matumizi ya silaha inawatia shaka wahariri wa Ujerumani. Mmojawao ni mhariri wa gazeti la “Ostthüringer Zeitung” la mjini Gera. Ameandika:
“Chama cha ETA kimekubali kuviacha vitendo vya kigaidi, lakini hakijaacha dai lake kutaka jimbo la Basque liwe huru. Kwa sababu hii migogoro mingine inatarajiwa kama katika mwaka 1999. Tofauti ya hivi sasa ni kuwa tangu miaka miwili iliopita Jose Luis Zapatero anayaiongoza Uhispania ni mwanachama wa Social Democrats anayependelea mageuzi. Ingawa Zapatero anakataa uhuru kwa jimbo la Basque kama mtangulizi wake Aznar, hata hivyo inaonekana kuwa atakubali kuongeza nafasi ya haki za jimbo hilo kujitawala lenyewe.”

Na hatimaye ni gazeti la “Frankfurter Neue Presse” linaloandika:
“Taarifa ya ETA ya kusitisha matumizi ya silaha ichukuliwe kwa uangalifu. Neno hili la “kusitisha” linaonyesha kuwa ETA kinatishia kutumia tena nguvu ikiwa mazungumzo na serikali ya Uhispania hayatafikia lengo la ETA, yaani jimbo la Basque lipate uhuru. Ingefaa waasi ETA kwanza waache kabisa ugaidi ili waaminike.”