Estonia yahimiza wanachama wa NATO kuongeza bajeti ya Ulinzi
27 Septemba 2023Akizungumza pembezoni mwa mkutano wa kila mwaka juu ya usalama wa eneo la Baltiki ulianza jana nchini Estonia, Bibi Kallas amesema ni muhimu kwa nchi nyingine za NATO kutanua matumizi ya sekta ya ulinzi kwa sababu kitisho cha usalama kimeongezeka na vita vimerejea barani Ulaya.
Mkutano huo wa mataifa ya Baltiki yanayojumuisha Latvia, Lithuania na Estonia, unafanyika chini ya kiwingu cha wasiwasi mkubwa wa usalama kwenye eneo hilo tangu Urusi ilipoivamia kijeshi Ukraine mwaka jana.
Soma pia:NATO: Hakuna ishara Urusi imeishambulia makusudi Romania
Waziri Mkuu huyo wa Estonia ameitaja nchi yake kuwa mfano ndani ya NATO akisema imepanga kupandisha kiwango cha bajeti yake ya ulinzi hadi kufikia asilimia 3.2 ya pato la taifa ifiakapo mwaka unaokuja.
Kwa miaka kadhaa sasa mengi ya mataifa yote 31 wanachama wa jumuiya wa jumuiya ya NATO wameshindwa kufikia lengola kutumia alau asilimia 2 ya pato jumla la taifa kwenye masuala ya ulinzi.