1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NATO yasema hakuna ishara za Urusi kuilenga Romania

Sylvia Mwehozi
8 Septemba 2023

Katibu Mkuu wa Jumuiya ya kujihami NATO Jens Stoltenberg, amesema hakuna ishara kwamba Urusi imefanya shambulio la makusudi dhidi ya mwanachama wake Romania.

https://p.dw.com/p/4W5jM
Jens Stoltenberg
Katibu Mkuu wa Jumuiya ya kujihami NATO Jens StoltenberPicha: Ludovic Marin/AFP/Getty Images

Katibu Mkuu wa Jumuiya ya kujihami NATO Jens Stoltenberg, amesema hakuna ishara kwamba Urusi imefanya shambulio la makusudi dhidi ya mwanachama wake Romania,baada ya mabaki ya ndege ya droni kupatikana karibu na mpake wake na Ukraine.

Stoltenberg amebainisha kuwa bila kujali matokeo ya uchunguzi unaoendelea, lakini kinachoshuhudiwa kwa hivi sasa ni kitisho cha mapigano na mashambulizi ya anga karibu na mipaka ya NATO.

Rais wa Romania Klaus Iohannis, alitoa wito wa uchunguzi wa haraka juu ya mabaki yanayoaminika kuwa ya droni yaliyogunduliwa kwenye ardhi yake kufuatia mashambulizi katika nchi jirani ya Ukraine.

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Antony Blinken, ambaye alikuwa ziarani Ukraine, amelijadili suala hilo katika mazungumzo ya simu na waziri mwenzake wa Romania Luminita Odobescu.