1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Donald Trump akataa mdahalo mwingine na Kamala Harris

13 Septemba 2024

Rais wa zamani wa Marekani, Donald Trump, amesema hatoshirki mdahalo mwingine wa televisheni na mpinzani wake, Kamala Harris. Ingawa kura za maoni zilionyesha kuwa Harris alishinda mdahalo wa kwanza.

https://p.dw.com/p/4kb8k
Uchaguzi Marekani
Mgombea wa urais wa Republican Donald Trump na mwenzake wa Democratic Kamala HarrisPicha: Alex Brandon/AP Photo/picture alliance

Trump alitoa msimamo huo baada ya yeye na Harris kurejea kwenye kampeni zao katika majimbo yenye maamuzi ambako yumkini kinyang'anyiro kikali cha kuingia ikulu ya White House kitaamuliwa mwezi Novemba. 

Harris amkaanga Trump kwenye mdahalo wa televisheni

Rais huyo wa zamani kupitia chama cha Republican alichapisha ujumbe kwenye mtandao wake akidai kuwa alishinda mdahalo wa Jumanne, ingawa uchunguzi wa maoni ulionesha Harris alishinda mdahalo huo uliotazamwa na watu milioni 67. 

Akizungumza kwenye mkutano wa kampeni katika jimbo la North Carolina, mgombea wa Democratic, Harris, alisisitiza kuwa wawili hao wanapaswa kujadiliana tena kabla ya uchaguzi wa Novemba 5.