1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

De Hoop Scheffer atoa mwito wa kuongezwa juhudi za NATO Afghanistan

17 Januari 2004
https://p.dw.com/p/CFiP
BRUSSELS: Katibu Mkuu wa Shirika la NATO Jap de Hoop Scheffer ameziita nchi zanachama za NATO ziongeze juhudi zao za misaada nchini Afghanistan. Mwenye kutaka ushindi katika vita dhidi ya ugaidi, lazima ainusuru Afghanistan, aliandika Bwana de Hoop Scheffer katika gazeti la Kijerumani BILD AM SONNTAG. Akasisitiza kuwa kutanuliwa kwa kikosi cha NATO nje ya mji mkuu Kabul ni uamuzi sahihi wa kisiasa na kijeshi. Ujerumani imetoa mchango mkubwa katika Afghanistan, alisisisita Katibu Mkuu huyo wa NATO.