1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

David Kay asema Iraq haina tena silaha za kuangamiza:

24 Januari 2004
https://p.dw.com/p/CFhO
WASHINGTON: Aliyekuwa mkuu hadi sasa wa wakaguzi wa silaha wa Kimarekani nchini Iraq, David Kay, amesema kwa maoni yake nchini Iraq hazitoweza tena kugunduliwa silaha za kuangamiza. Bwana Kay alisema hayo baada ya kujiuzulu kutoka wadhifa huo. Mfuasi wake atakuwa mkaguzi wa zamani wa silaha wa UM, Charles Duelfer. Naye Bwana Juelfer hivi karibuni tu alisema hana hakika iwapo Marekani na washirika wake wataweza kugundua silaha za kuangamiza za kikemikali na kibiolojia huko Iraq. Msemaji wa Ikulu mjini Washington alisema Marekani inaendelea kushikilia kuwa Iraq ilikuwa na programu ya silaha za kuangamiza na ikificha silaha marufuku. Shutuma za Marekani kwamba Iraq inadhibiti silaha za kuangamiza zilikuwa chanzo kikubwa kabisa kwa uamuzi wa Rais George W. Bush wa kuipiga vita Iraq.