1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

DARFUR: Mwito watolewa madai ya ubakaji yachunguzwe

6 Aprili 2007
https://p.dw.com/p/CCC2

Mwakilishi wa maswala ya haki za binadamu wa umoja wa mataifa ametoa mwito wa kuanzishwa uchunguzi kuhusu madai ya ubakaji na kutoweka kwa watu katika jimbo la darfur nchini Sudan.

Kamishna wa haki za binadamu wa umoja wa mataifa Louise Arbour amesema serikali ya Khartoum ina wajibu wa kufanya uchunguzi kuhusu malalamiko 15 dhidi ya wanajeshi wanaotuhumiwa kuwabaka wanawake katika vijiji kadhaa huko Darfur jimbo linalokabiliwa na machafuko.

Ineripotiwa kuwa wasichana wa umri wa miaka 13 na wanawake waja wazito ni wahanga wa ubakaji.

Wakati huo huo bwana Arbour ameitaka serikali ya Sudan kuchunguza pia kutoweka kwa watu 19 wanaodaiwa walitekwa na askari wa Sudan.