1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

DAR ES SALAAM: Makubaliano ya amani yatiwa saini

8 Septemba 2006
https://p.dw.com/p/CDEa

Burundi na kundi la mwisho la waasi zimetia saini makubaliano ya kusitisha mapigano.Rais Pierre Nkurunziza wa Burundi, aliekuwa kiongozi wa waasi wa Kihutu hapo zamani na Agathon Rwasa wa kundi la FNL ambae pia ni Mhutu,walitia saini makubaliano hayo siku ya Alkhamisi,mjini Dar-es- salaam,Tanzania.Mkataba huo wa amani ulitiwa saini mbele ya wapatanishi Afrika Kusini na viongozi wengine wa Kiafrika.Kundi la FNL lilikataa kutia saini makubaliano ya amani yaliyopatikana miaka sita ya nyuma.